KIUNGO wa timu ya Taifa ya Ufaransa, Lassana Diarra atalazimika kuzikosa fainali za Kombe la Dunia kutokana na matatizo ya tumbo yanayomkabili.
Hatua hiyo imekuja baada ya kiungo huyo wa Real Madrid kushindwa kufanya mazoezi kwa muda wa siku tatu mfululizo na timu ya Taifa ya Ufaransa.
“Ndiyo, mara nyingi huwa ni pigo unapompoteza mchezaji. Ni vigumu kwa sababu hatukutaka iwe hivyo,” alisema kocha wa timu hiyo, Raymond Domenech.
“Ni vigumu kwake kwa sababu nafahamu jitihada alizokuwa amezielekeza katika fainali hizi na ni mmoja wa wachezaji ambao wameiwezesha timu kucheza kama inavyocheza na morali waliyonao," aliongeza kocha huyo.
Naye msemaji wa timu hiyo ya Taifa, Francois Manardo alisema kwa mara ya kwanza Diarra kuhisi maumivu ilikuwa ni Jumatano, hali ambayo ilimfanya ashindwe kufanya mazoezi na wenzake.
Manardo alisema kuwa Diarra anahitaji kupumzika kipindi kisichojulikana ili kuuguza matatizo hayo hayo.
Hadi sasa Diarra ameweza kuichezea Ufaransa mara 27 tangu alipoanza kung'ara miaka mitatu iliyopita.

No comments:
Post a Comment