
Ndoto za mabingwa wa soka nchini Uingereza Chelsea za kutaka kumsajili kiungo wa kimataifa toka nchini Croatia, Luka Modric zimeota mbawa baada ya kuingo huyo kusaini mkataba wa muda wa miaka sita na klabu yake ya Tottenham.
Sababu kubwa zilizotolewa na uongozi wa klabu ya Tottenham zilizopelekea kiungo huyo kupewa mkataba wa muda mrefu zimetokana na mchango wake aliouonyesha msimu uliopita ambao kwa asimilia kubwa uliisaidia klabu hiyo kupata nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi.
No comments:
Post a Comment