
Uongozi wa klabu ya Real Madrid hii leo umemtambulisha rasmi Jose Mourinho kuwa meneja mpya wa klabu hiyo yenye kiu ya ubingwa wa muda wa misimu miwili mfululizo.
Mourinho ametambulishwa hadharani kwenye makao makuu ya klabu hiyo huko St Berabaeu na mkurugenzi wa michezo Real Madrid Jorge Valdano.
Akizungumza kwenye mkutano huo wa waandidhi wa habari Valdano amesema wamempokea kwa shauku kubwa meneja huyo mwenye umri wa miaka 47 na wanaamini atafikia malengo wanayoyakusudia.
Kwa upande wake Mourinho aliejiunga na klabu hiyo kwa mkataba wa miaka minne amesema yupo tayari kwa ushindani wa kisoka ambao ana imani atakutana nao kwenye michuano mbali mbali atakayoshiriki msimu ujao.
Amesema anajiamini kwa uwezo wake alionao huku akiwataka waandishi wa habari ulimwengu mzima kutambua Mourinho atabaki kuwa Mourinho na kamwe hatobadilika na ndio maana jina leke la utani la Special One linaendelea kudumu.
Alipoulizwa juu ya kiungo wa klabu hiyo Cristiano Ronaldo, amesema ni mchezaji mzuri kwa upande wa timu yake ya taifa ya Ureno sambamba na klabu pia, hivyo anategemea kumtumia katika taratibu za kusaka mafanikio kuanzia msimu ujao.
Kutambulishwa Mourinho kuwa meneja mpya wa klabu ya Real Madrid kunaifanya klabu hiyo kufikisha idadi ya mameneja wanane ndani ya miaka saba iliyopita.
No comments:
Post a Comment