KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, June 1, 2010

UCHE NA ANICHEBE NJE.


Mshambuliaji wa klabu ya Real Zaragoza ya nchini Hispania Uche Ikechukwu pamoja na Victor Anichebe wa klabu ya Everton wameachwa kwenye kikosi cha wachezaji 23 cha timu ya taifa ya Nigeria.

Uche ametemwa katika kikosi hicho huku akiacha kumbu kumbu ya kuibuka mchezaji aliefunga mabao mengi wakati timu ya taifa ya Nigeria ilipokua ikisaka nafasi ya kushiriki kwenye fainali za kombe la dunia za mwaka 2010.

Wakati Uche na Anichebe wakiachwa katika kikosi hicho beki na nahodha wa klabu ya Everton Joseph Yobo mshambuliaji wa klabu ya Portsmouth Nwankwo Kanu pamoja na kiungo wa klabu ya Chelsea John Obi Mikel wamejumuishwa kwenye kikosi hicho cha Super Eagles.

Baadhi ya wachezaji wengine waliojumuishwa kwenye kikosi hicho ni John Utaka wa klabu ya Portsmouth, Yakubu Aiyegbeni , Dickson Etuhu wa klabu ya Fulham pamoja na Danny Shittu wa klabu ya Bolton Wanderers .

Timu ya taifa ya Nigeria imepangwa kwenye kundi la pili lenye timu za Argentina, Ugiriki pamoja na Korea Kusini.

No comments:

Post a Comment