KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, June 3, 2010

Andrea Cossu YU MBIONIO KUELEKEA SOUTH AFRICA.


Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Italia Marcelo Lippi huenda akamuita kiungo wa klabu ya Cagliari Andrea Cossu kwenye kikosi chake cha wachezaji 23 ambacho kipo tayari kutetea ubingwa wa dunia kwenye fainali za kombe la dunia huko nchini Afrika kusini.

Lippi anategemea kufanya maamuzi hayo huku siku za kuweka wazi vikosi vya timu zote 32 zitakazoshiriki fainali za kombe la dunia mwaka huu ukimalizika toka June mosi.

Sababu kubwa ya kocha huyo kutarajia kumuongeza kikosini Andrea Cossu ni kufuatia kuumia goti kwa kiungo wa klabu ya Juventus Mauro Camoranesi ambae tayari alishatajwa kwenye kikosi cha wachezaji 23.

Hata hivyo Lippi anapewa msukumo wa kumuita Andrea Cossu kufuatia kanuni za FIFA ambazo zinaeleza timu shiriki zinaweza kumuongeza mchezaji asiezidi mmoja endapo kutakua na majeruhi kikosini kabla ya mchezo wa ufunguzi haujachezwa.

Kufuatai sababu hiyo Lippi bado ana nafasi ya kuuwahi muda wa kumuita kiungo huyo wa klabu ya Cagliari kabla ya mchezo wa kwanza ambao utashuhudia Afrika kusini wakifungua fainali za kombe la dunia kwa kucheza na timu ya taifa ya Mexico.

No comments:

Post a Comment