Uongozi wa klabu ya Liverpool umetangaza kuondoka kwa aliekua meneja wao Rafael Benitez kwa muda wa miaka sita iliyopita.
Benitez, mwenye umri wa miaka 50, ameondoka klabuni hapo kufuatia kuwa na msimu mbovu wa mwaka 2009-10 ambao ulimalizika kwa kushuhudia Liverpool wakimaliza katika nafasi ya saba kwenye msimamo wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza.
Kuondoka kwa meneja huyo toka nchini Hispania, sasa kunatoa nafasi kwa mkurugenzi mkuu wa klabu ya Liverpool Christian Purslow kusaidiana na meneja wa zamani Kenny Dalglish kuanza mchakato za kumsaka meneja mpya.
itakumbukwa kuwa Benitez alijiunga na klabu ya Liverpool Mwezi June mwaka 2004 mara baada ya kuondoka kwa Gerard Houllier, na amefanikiwa kuizawadia klabu hiyo ubingwa wa ulaya pamoja na ubingwa wa kombe la FA.

No comments:
Post a Comment