KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, June 3, 2010

CAPELLO KUPETA MPAKA 2012



Hatimae kocha mkuu wa timu ya taifa ya Uingereza Fabio Capello amefanikiwa kuboreshewa mkataba wake ambao sasa utafikia kikomo mwishoni mwa fainali za mataifa ya Ulaya zitakazochezwa nchini Ukraine mwaka 2012.

Cappello mwenye umri wa miaka 63 amekubali kusaini maboresho ya mkataba wake, baada ya kufikia muafaka na viongozi wa chama cha soka nchini Uingereza mbao walishtushwa na taarifa za kutaka kujiunga kwake na klabu ya Inter Milan ya nchini kwao Italia.

Cappelo amesema hatua ya kuboreshewa mkataba wake, imempa mwanya wa kujisikia faraja huku akibainisha wazi kwamba hatua hiyo itamuwezesha kufanya kazi kwa usalama mpaka mwaka 2012.

Amesema wakati wote alitamani kuendelea kusalia nchini Uingereza lakini kikwazo kilikua ni maboresho ya mkataba wake na hii leo anashukuru mungu kikwazo hicho kimeondoka.

Kukamilika kwa hatua ya kusaini maboresho ya mkataba wa Capello, sasa kunavunja mipango ya uongozi wa klabu ya Inter Milan ambao ulikuwa kwenye harakati za kumnasa mara zitakapomalizika fainali za kombe la dunia mwaka huu huko nchini Afrika kusini.

Sababu kubwa ya Capello kutakiwa nyumbani katika klabu Inter Milan ni kufuatia kuondoka kwa Jose Mourinho alietangazwa kuwa meneja mpya wa klabu ya Real Madrid mwanzoni mwa juma hili.

No comments:

Post a Comment