KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, June 2, 2010

BARCA WATUMA OFA ARSENAL !!


Uongozi wa klabu bingwa nchini Hispania Fc Barcelona umesema upo tayari kuanza taratibu za kumuhamisha kiungo an nahodha wa klabu ya Arsenal ya Uingereza Cesc Fabregas.

Mabingwa hao wa Hispania wameweka wazi utaratibu huo kupitia vyombo mbali mbali vya habari baada ya msimu wa usajili wa mwaka 2010-11 kufunguiliwa rasmi hapo jana huku wakiwa na imani kubwa ya kufanikisha taratibu hizo.

Utaratibu huo wa Barcelona tayari umeshaingia mashaka kupitia kwa mashabiki mbali mbali ulimwenguni ambao wanadhani huenda ukawagharimu kiasi kikubwa cha fedha kufuatia uongozi wa klabu ya Arsenal kuhitaji fedha za kufanya usajili wa wachezaji.

Hata hivyo uongozi wa klabu ya Barcelona tayari umeshajinadi kutoa kiasi cha paund million 30 ambazo zitatumika kama ada ya uhamisho wa kiungo huyo, kiasi ambacho siku za hivi karibuni kilikataliwa na meneja wa klabu ya Arsenal Arsene Wenger ambae alidai Fabregas ataondoka huko Emirates kwa dili la paund million 80.

Kikwazo kingine ambacho kinahisiwa huenda kikawapa wakati mgumu wa viongozi wa Barcelona ni mkataba mzito wa miaka minane uliosainiwa na Fabregas toka mwaka 2006, ambao ndio unamuongoza katika taratibu za kuuzwa kwake.

Ikumbukwe kuwa mwishoni mwa msimu wa mwaka 2009-10 Cesc Fabregas alimueleza wazi meneja wake Arsene Wenger kwamba yu radhi kuondoka kwenye himaya yake kwa sasa.

No comments:

Post a Comment