Kocha mkuu wa timu ya taifa ya nchi hiyo Fabio Capello amewashtua wengi katika uteuzi wa kikosi chake kufuatia kumuacha winga wa klabu ya Arsenal Theo Walcot ambae alikuwa mmoja wa wachezaji walioisaidia timu hiyo kutinga kwenye fainali za kombe la dunia.
Walcot ambae alifunga mabao matatu kwenye mchezo wa kufuzu dhidi ya timu ya taifa ya Croatia ameachwa kwenye kikosi huku sababu kubwa ikitajwa kutotumika vyema kwenye klabu yake ya Arsenal kufuatia upasuaji wa bega aliofanyiwa kati kati ya msimu wa mwaka 2009-10.
Wachezaji wengine walioachwa kwenye kikosi cha wachezaji 23 cha Uingereza ni Darren Bent, Adam Johnson, Scott Parker, Michael Dawson, Leighton Baines pamoja na Tom Huddlestone.
Kikosi kamili kilichotajwa ni kwa upande wa
Makipa: Joe Hart (Manchester City), David James (Portsmouth), Robert Green (West Ham).
Mabeki: Jamie Carragher (Liverpool), Ashley Cole (Chelsea), Rio Ferdinand (Manchester United), Glen Johnson (Liverpool), Ledley King (Tottenham), John Terry (Chelsea), Matthew Upson (West Ham), Stephen Warnock (Aston Villa).
Viungo: Gareth Barry (Manchester City), Michael Carrick (Manchester United), Joe Cole (Chelsea), Steven Gerrard (Liverpool), Frank Lampard (Chelsea), Aaron Lennon (Tottenham), James Milner (Aston Villa), Shaun Wright-Phillips (Manchester City).
washambuliaji: Peter Crouch (Tottenham), Jermain Defoe (Tottenham), Emile Heskey (Aston Villa), Wayne Rooney (Manchester United).

No comments:
Post a Comment