KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, June 8, 2010

BENITEZ ANAKARIBIA.


Aliekua meneja wa klabu ya Liverpool Rafa Benitez huenda akatangazwa kuwa meneja wa klabu ya Inter Milan ndani ya saa 24 zijazo.

Taarifa za Benitez kukaribiwa kuwa meneja wa klabu hiyo bingwa barani Ulaya, zimeonyesha matumaini kufuatia raisi wa klabu ya Inter Milan Massimo Moratti kuthibitisha safari ya kwenda kuzungumza na Mspaniola huyo alie mapumzikoni huko kwenye kisiwa cha Sardinia kilichopo nchini Italia.

Moratti amesema sababu kubwa ya kutarajia kuanza mazungumza na Benitez ni baada ya kuonekana ndie meneja aliefikia vigezo ambavyo vinawashawishi kumrithi Jose Mourinho, alietimkia Real Madrid.

Hata hivyo imeelezwa kuwa Benitez amesalia kwenye kinyang’anyiro cha umeneja wa Inter Milan sambamba na aliekua meneja wa klabu ya Real Madrid Manuel Pellegrini.


No comments:

Post a Comment