KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, June 8, 2010

POUND MILION 50 KUMNG'OA CESC ARSENAL !


Hatimae uongozi wa klabu ya Arsenal umeamua kuanika wazi bei ya kumuuza nahodha na kiungo wao wa kimataifa toka nchini Hispania Cesc Fabregas, anaewaniwa na klabu bingwa nchini Hispania Fc Barcelona.

The Gunners wamebainisha wazi bei ya kumuuza kiungo huyo huku zikiwa zimepita siku kadhaa baada ya kutangaza Fabregas hauzwi kufuatia ofa iliyotumwa na viongozi wa FC Barcelona.

Bei iliyotangazwa na Arsenal ni kiasi cha paund million 50 ambacho kinadhaniwa kuwa tosha kumng’oa kiungo huyo huko Emirates kwa klabu yoyote inayomuhitaji kuanzia sasa.

Hata hivyo imeelezwa kuwa Arsenal wamepata jeuri ya kutangaza bei hiyo baada ya kuwa na uhakika wa kumsajili kiungo wa klabu ya Chelsea Joe Cole ambae yu huru toka msimu wa mwaka 2009-10 ulipomalizika.

Pamoja na kutangazwa kwa bei hiyo taarifa toka nchini Hispania zimeeleza kuwa bado uongozi wa Fc Barcelona umeendelea kushikilia msimamo wake wa kutaka kumsajili Fabregas kwa ada ya paund million 35.

No comments:

Post a Comment