
Nahodha na mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ivory Coast Didier Drogba hii leo alitarajiwa kujiunga na wachezaji wenzake baada ya jana kufanyiwa upasuaji kwenye jeraha la mkono wake.
Mshambuliaji huyo alitarajiwa kujiunga na wenzake huku matumaini ya kuchezeshwa kwenye kikosi cha kwanza cha Tembo wa Afrika ya Magharibi kitakachocheza mchezo wake wa kwanza dhidi ya timu ya taifa ya Ureno mjini Port Elizabeth mwishoni mwa juma hili yakipanda kwa asilimia kubwa.
Msemaji wa timu ya taifa ya Ivory Coast Roger Kouassi ameeleza kuwa Dogba mpaka mapema hii leo alikua akiendelea vyema baada ya kutumia siku tatu akiwa kwenye moja ya hospitali huko nchini Australia.
Itakumbukwa kuwa Drogba alivunjika mfupa wa mkono wake wa kulia mwishoni mwa juma lililopita alipokua kwenye mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya timu ya timu ya taifa ya Japan.
No comments:
Post a Comment