Wakala wa kiungo wa klabu ya Barcelona Yaya Toure amesema mchezaji huyo kwa sasa yu tayari kujiunga na klabu yoyote inayocheza ligi kuu ya soka nchini Uingereza.
Yaya Toure ambae kwa sasa yupo kwenye timu ya taifa lake la Ivory Coast akijiandaa na fainali za kombe la dunia, tayari ameonyesha dhamira hiyo toka mwishoni mwa msimu wa mwaka 2009-10 huku klabu ya Manchester City, Manchester United pamoja na Arsenal zikiwa mstari wa mbele katika harakati za kumgombea.
Dimitri Seluk wakala wa kiungo huyo ametanabai kwamba tayari kuna moja ya vilabu hivyo ipo kwenye mazungumzo ya kumuhamisha mchezaji huyo na anaamini mara bada ya fainali za kombe la dunia utaratibu wa uhamisho wake utafahamika.
Yaya Toure alijiunga na klabu ya Barcelona akitokea kwenye klabu ya Monaco ya nchini Ufaransa kwa ada ya uhamosho wa Euro million nane mwezi June mwaka 2007.

No comments:
Post a Comment