Meneja wa klabu ya Man City Roberto Mancini ametangaza kuwa mbioni kuwatema wachezaji wake watatu ambao hawakumridhisha kisoka kwenye msimu wa mwaka 2009-10.
Mancini ametangaza kuwatema wachezaji hao ambao ni Martin Petrov, Benjani Mwaruwari pamoja na Sylvinho huku vyanzo mbali mbali vya habari vikieleza yu mbioni kuwasajili wachezaji wengine watakaoziba mapengo yao.
Wachezaji hao watatu walisajiliwa na klabu ya Man City chini ya mameneja waliopita kabla ya kuajiriwa kwa Roberto Mancini, hali ambayo iliwafanya kuonekana mzigo katika kampeni ya kuwania nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi kuu nchini Uingereza msimu uliopita.
Martin Petrov aliecheza michezo 57 na kuipachikia Man city mabao 15 alisajiliwa na Sven-Goran Eriksson mwaka 2007akitokea Atletico Madrid ya nchini Hispania.
Mara kadhaa winga huyo wa kimataifa toka nchini Bulgaria amekuwa akishindwa kucheza soka kwa kipindi kirefu cha msimu kufuatia kuwa majeruhi hatua ambayo imetajwa kuwa sababu ya kutarajiwa kutemwa kwake.
Mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Zimbabwe Benjani Mwaruwari nae alisajiliwa na Sven-Goran Eriksson mwezi januari mwaka 2008 akitokea kwenye klabu ya Portsmouth.
Sababu ya kutarajia kutemwa kwake ni kufautia kuonyesha kiwango cha chini hali ambayo ilimshawishi Mancini kumtoa kwa mkopo kwenye klabu ya Sunderland.
Kwa upande wake Mbrazil Sylvinho mwenye umri wa miaka 36 aliejiunga na klabu hiyo msimu uliopita chini ya meneja Mark Hughes nae ameshindwa kuonyesha uwezo kama alivyokua Fc Barcelona hali ambayo imemfanya kucheza michezo tisa kwa muda wa msumu mzima.

No comments:
Post a Comment