Mshambuliji na nahodha wa timu ya taifa ya Ivory Coast Didier Drogba huenda asionekane kwenye fainali za kombe la dunia zilizosaliwa na siku sita kabla ya kuanza kwake huko nchini Afrika kusini.
Drogba ameingia katika hali hiyo ya sintofahamu kufuatia kuumia mkono kwenye mchezo wa kujipima ubavu uliochezwa mapema hii leo dhidi ya timu ya taifa ya Japan iliyokubali kisago cha mabao mawili kwa sifuri.
Akithibitisha taarifa za mshambuliaji huyo kuwa mashakani kucheza fainali za kombe la dunia beki wa klabu ya Man City Kolo Toure, amesema kwa mara ya mwisho alipozungumza na Drogba mara baada ya kutolewa nje ya uwanja katika dakika ya 15, alimwambia ndoto zake za kucheza kwenye fainali hizo zimekwisha.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 32 alijikuta akiangukia mkono mara baada ya kupata upinzani mkali toka kwa beki wa Japan Marcus Tulio Tanaka na baada ya hapo alikimbizwa Hospitali.
Hata hivyo taarifa zilizotolewa na msemaji wa timu ya taifa ya Ivory Coast Eric Kacou mara baada ya mshambuliaji huyo kufikishwa Hospitali zimeeleza kuwa Drogba amebainika amevunjika mkono.

No comments:
Post a Comment