KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, June 4, 2010

REINA ASIKITIKA !!!!!!!!!!!


Kipa nambari moja waa kikosi cha klabu ya Liverpool Jose Pepe Reina amesikitishwa na hatua ya kuondoka kwa aliekua meneja wa klabu hiyo Rafael Benitez.

Jose Pepe Reina ambae kwa sasa yupo kambini na wachezaji wenzake wa Hispania wakijiandaa na fainali za kombe la dunia amesema amesikitishwa na utaratibu huo ambao anadhani hajaamuliwa kwa wakati muafaka.

Kipa huyo ametanabai kwamba muda wa Beniztez kuondoka Liverpool haukustahili kuwa hivi sasa kutokana na umoja aliokuwa ameutengeneza kwenye kikosi chake ambacho kilimaliza msimu kikiwa kwenye nafasi ya saba.

Reina, ambae alisajiliwa na Benitez mwaka 2005 akitokea kwenye klabu ya Villareal ya nchini kwao Hispania na kufanikiwa kucheza michezo 182 akiwa na klabu ya Liverpool amesema daima atamuheshimu na kumkumbuka meneja huyo kwa mema aliyomfanyia.

Hata hivyo Reina ameongeza kuwa anaamini meneja wa zamani wa klabu ya Liverpool Kenny Dalglish kwa kusaidiana na ngazi za juu za uongozi watampata meneja ambae ataweza kuziba pengo lililoachwa na Benitez.

No comments:

Post a Comment