KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, June 8, 2010

FERDINAND KUENDELEA KUBAKI AFRIKA KUSINI.


Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Uingereza Fabio Capello nae ameamua kutangaza kuendelea kubaki na beki wa klabu ya Man utd Rio Ferdinand ambae ni majeruhi wa goti.

Capello amesema Rio Ferdinand ambae tayari nafasi yake imeshachukuliwa na Michael Dawson bado ni sehemu ya timu hivyo ameona ni bora aendelee kuwepo nchini Afrika kusini kwa lengo la kuwapa hamasa wachezaji wenzake.

Rio Ferdinand alipata maumivu ya goti alipokua mazoezini mwishoni mwa juma lililopita wakati akijaribu kuokoa hatari katika upande aliokua akiutetea.

No comments:

Post a Comment