KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, June 7, 2010

ROBEN KUBAKI KIKOSINI !!!


Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Uholanzi Bert van Marwijk amesema mshambuliaji wa klabu ya Bayern Munich Arjen Robben ataendelea kuwepo kikosini licha ya kuumia nyama za paja mwishoni mwa juma lililopita.

Kocha huyo amesema Roben ataendelea kusalia kikosini licha ya jana kufanyiwa vipimo na kubainika huenda ikamchukua muda mrefu kurejea katika hali yake ya kawaida.

Wakati kocha akisisitiza jambo hilo la kuendelea kuwa sambamba na Roben, nao uongozi wa chama cha soka nchini uholanzi umetia neo kwa kubainisha wazi kwamba daima hauwezi kuingilia maamuzi yaliyotolewa na Bert van Marwijk.

Itakumbukwa kuwa Arjen Roben aliumia katika dakika za lala salama za mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Hungury ambapo Uholanzi walipata ushindi wa mabao sita kwa moja.


No comments:

Post a Comment