KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, June 1, 2010

KIPENZI CHA WENGI CHAACHWA AFIKA KUSINI.





Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Afrika kusini Carlos Alberto Parreira amemuacha mshambuliaji wa klabu ya West Ham Benni McCarthy kwenye kikosi cha wachezaji 23 kitakaoshiriki kwenye fanali za kombe la dunia mwaka huu.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 32 anaeshikilia rekodi ya kupachika mabao mengi akiwa na timu ya taifa ya Afrika kusini ameachwa na kocha huyo huku sababu kubwa ikitajwa ni kushuka kwa kiwango chake pamoja na kuongezeka uzito wa mwili.

Mbali na McCarthy pia Perreira amewaacha wachezaji watano kwenye kikosi chake ambao ni pamoja na kipa wa klabu ya Arminia Bielefeld ya nchini Ujerumani Rowen Fernandez, beki wa klabu ya PAOK ya nchini Ugiriki Bryce Moon, Innocent Mdledle, pamoja na Franklin Cale.

Wachezaji mashuhuri waliotajwa kwenye kikosi hicho ni kiungo wa klabu ya Everton Steven Pienaar, kiungo wa klabu ya Fulham Kagiso Dikgacoi pamoja na beki wa klabu ya Portsmouth Aaron Makoena ambae jana ametimiza idadi ya michezo 100 aliyocheza akiwa na timu ya taifa ya Afrika kuisni iliyotoa kisago cha mabao matano kwa sifuri kwa timu ya taifa ya Guatemala.

Wengine ni waliotwa na Perreira ni Katlego Mphela (Mamelodi Sundowns), Siyabonga Nomvete (Moroka Swallows) Teko Modise (Orlando Pirates), MacBeth Sibaya (Rubin Kazan), pamoja na Siphiwe Tshabalala (Kaizer Chiefs).

Timu ya taifa ya Afrika kusini itafungua fainali za kombe la dunia June 11 kwa kucheza na timu ya taifa ya Mexico na baadae itacheza na timu ya taifa ya Ufaransa pamoja na Uruguay.

No comments:

Post a Comment