KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, June 1, 2010

KONE NA AKALE KUCHOMA MAHINDI.



Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Ivory Coast Sven-Goran Eriksson amemuacha mshambuliaji wa klabu ya Lekhwiya ya nchini Qatar Bakary Kone pamoja na Kanga Akale wa klabu ya Recreativo Huelva ya nchini Hispania.

Erickson aliepewa jukumu la kuwanoa tembo hao wa Afrika ya magharibi pia amewaacha kikosni Emerse Fae, Gilles Yapi Yapo pamoja na Traore Lacina huku akimrejesha Christian Koffi Ndri wa klabu ya Sevilla ya Hispania ambae aliachwa mwezi januari kwenye fainali za kombe la mataifa ya Afrika kwa sababu za kinidhamu.

Baadhi ya wachezaji wengine waliotajwa kwenye kikosi hicho cha Ivory Coast kilichosaliwa na wachezaji 23 ni pamoja na Didier Drogba, Salamon Kalou, Aruna Dindane pamoja na Seydou Doumbia

Timu ya taifa ya Ivory Coast imepangwa kwenye kundi la saba lenye timu za Brazil, Ureno pamoja na Korea Kaskazini.

No comments:

Post a Comment