KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, June 7, 2010

MUNTARI AITIA HOFU KAMBI YA GHANA.


Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Ghana Milovan Rajevac amesema bado yupo kwenye hali ya sintofahamu kama atamtumia kiungo wa klabu ya inter Milan ya Italia Sulley Muntari kwenye fainali za kombe la dunia ama la.

Muntari anamuumiza kichwa kocha huyo huku ikielezwa kuwa uwezekano wa kuchezeshwa kweney fainali za kombe al dunia mpaka hivi sasa ni mdogo ambapo hata hivyo imeenleza kuwa jopo la madaktari wa timu ya taifa ya limekua likifanya shughuli ya kuhakikisha kiungo huyo anarejea katika hali yake ya kawaida.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 25 alipatwa na majertuhi kwenye mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya timu ya Uholanzi ambao ulimalizika kwa timu ya taifa ya Ghana kulambishwa shubiri ya mabao manne kwa moja.

Hata hivyo tayari Muntari alikua ameshatajwa kuwa mbadala wa Michael Essien ambae hatocheza fainali za kom,be la dunia mwaka huu, hatua mbayo yadhaniwa kuwa chanzo cha kocha Milovan Rajevac kujiuliza ni lini kiumngo huyo atarejea katika hali yake kisawa sawa.

No comments:

Post a Comment