KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, August 16, 2010

BADO NIPO NIPO SANAAAAAAA.


Mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Uingereza Peter Crouch amesema badi ni mwenye furaha huko White Hert Lan yalipo makao makuu ya klabu yake ya sasa Tottenham Hotspours.

Peter Crouch ametoa kauli hiyo baada ya kuandamwa na taarifa za kutaka kuuzwa na meneja wake Harry Rednapp katika vilabu vilivyonyesha nia ya kutaka kumsajili katika kipindi hiki cha usajili.

Amesema mazingira ya klabu hiyo ameyapenda na hana budi kusema ahsante kwa mashabiki wa Spurs ambao kila leo wamekua wakimuonyes mapenzi ya dhati hivyo suala la kuhama litamuweka katika hali ya simanzi.

Mshambuliaji huyo pia maeongeza kwamba mbali na kutaka kubaki klabuni hapo, pia ana uchu wa kuisaidia Spurs kufanya vyema katika michuano ya ligi ya mabingwa barani ulaya msimu huu baada ya kuwa miongoni mwa wachezaji walioiwezesha klabu hiyo kucheza mashindano hayo makubwa barani Ulaya katika ngazi ya vilabu.

No comments:

Post a Comment