KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, August 26, 2010

BEBE ASHINDWA KUMKUNA BABU.


Mshambuliaji mpya wa klabu ya Man Utd Tiago Manuel Dias Correia Bebe ameshindwa kumridhisha meneja wa klabu hiyo Sir Alex Ferguson anapokua mazoezini.

Hatua hiyo ya kushindwa kumridhisha babu huyo wa kiscotish imemfanya Tiago Manuel Dias Correia Bebe kutokupewa nafasi katika kikosi kinachoshiriki ligi kuu ya soka nchini Ungereza.

Mbali na kutokupewa nafasi katika kikosi hicho Tiago Manuel Dias Correia Bebe pia amekosa nafasi hata katika kikosi cha wachezaji wa akiba kilichocheza na Man city siku mbili zilizopita.

Hata hivyo imeelezwa kuwa meneja wa klabu ya Man utd Sir Alex Ferguson alimsajili mchezaji huyo pasipo kumuona kwa jicho la yakini zaidi ya kumuona kupitia televisheni huku msukumo mkubwa ukitoka kwa msaidizi wake wa zamani Carlos Queiroz.

Tiago Manuel Dias Correia Bebe amesajiliwa na Man utd kwa ada ya uhamisho wa paund million 7, akitokea nchini kwao Ureno katika klabu ya Vitória de Guimarães.

No comments:

Post a Comment