KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, August 24, 2010

NI VIGUMU KUIKTAA ARSENAL.


Beki wa kimataifa toka nchini Ufaransa Sebastien Squillaci amesema katu asingeweza kumkatalia meneja wa klabu ya Arsenal Arsene Wenger ambae amedhamiria kumsajili akitokea Sevilla Fc ya nchini Hispania.

Beki huyo ambae hii leo anatarajiwa kukamilisha taratibu za kujiunga na klabu ya Arsenal, amesema meneja huyo kwake ni chaguo la kwanza na aliamini ipo siku angecheza akiwa chini yake.

Amesema kutarajia kujianga Arsenal saa chache zijazo kwake ni kukamilisha ndoto alizokua nazo siku nyingi na anaamini atakisaidia kikosi cha klabu hiyo kufikia malengo ya kufanya vyema msimu huu.

Katika kuonyesha ni kweli Sebastien Squillaci alikua na dhamira ya dhati ya kujiunga na Arsene Wenger amesema alididriki kukataa kuichezea klabu yake ya Sevilla katika mchezo wa Super Cup dhidi ya Barcelona sambamba na mchezo wa ligi ya mabingwa barani ulaya dhidi ya FC bragha juma lililopita.

Nae kiungo wa kimataifa toka nchini Ivory Coast pamoja na klabu ya Sevilla ya nchini Hispania Alain Didier Zokora amesema Sebastien Squillaci anafaa kuitumikia Arsenal kutokana na mfumo wa uchezaji wa klabu hiyo.

Alain Didier Zokora amesema mfumo uchezaji wa klabu ya Arsenal ni mwepesi hivyo anaamini beki huyo amefanya maamzui sahihi ya kukubalia kijiunga na washika bunduki hao wa Ashburton Grove.

No comments:

Post a Comment