KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, August 24, 2010

SAM ALLARDYCE AMTAMANI.


Meneja wa klabu ya Blackburn Rovers Sam Allardyce amekata tamaa ya kumsajili kiungo wa kimataifa toka nchini Uingereza na klabu ya LA GALAX ya nchini Marekami David Beckham katika kipindi hiki.

Sam Allardyce alikua na mipango ya kumsajili kiungo huyo kufuatuia ahadi aliziopewa na bosi wake mtarajiwa Ahsan Ali Syed aliepania kuwekeza katika klabu hiyo ya huko Ewood Park.

Allardyce amesema matumaini ya kufanyika kwa usajili huo yamefifia kufuatia muda wa usajili kuzidi kuyoyoma huku mmiliki huyo akiwa bado hajakamilisha taratibu za uwekezaji.

amesema ni kweli anatamani kumsajili Beckham na lingekuwa jambo zuri sana kulikamilisha katika kipindi hiki ambacho anadai wachezaji wake wengi wanahitaji kujifunza kutoka kwa wakongwe.

Katika hatua nyingine Sam Allardyce ana matumaini ya kuuwahi muda wa usajili kwa kumsajili mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Bulgaria Ivelin Popov anaeichezea klabu ya Litex Lovech.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 22 anatarajiwa kuelekea huko Ewood Park, kwa lengo la kuboresha safu ya ushambuliaji ambayo Sam Allardyce amedai inahitaji usaidizi.

Akizungumzia hatua hiyo Sam Allardyce amesema mchezaji huyo bado hawajamsajili na amesikitishwa na taarifa za vyombo vingi vya habari kudai kwamba mshambuliaji huyo tayari amesshasajiliwa.

No comments:

Post a Comment