KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, August 18, 2010

BELLAMY AJIUNGA NA CARDIFF


Winga wa kimataifa toka nchini Wales Craig Bellamy amesema hajisikii vibaya kuondoka Eastland yalipo makao makuu ya klabu yake ya zamani Manchester City.

Craig Bellamy amelitghibisha hilo alipozungumza na waandishi wa habari baada ya uhamisho wake wa mkopo wa muda mrefu wa kujiunga na klabu ya nyumbani kwao ya Cardiff City kukamilika.

Craig Bellamy amesema hajisikii vibaya kutokana na maisha mazuri aliyoishi na wachezaji, mashabiki pamoja na viongozi wa klabu hiyo iliyopania kufanya vyema katika msimu huu wa soka.

Hata hivyo winga huyo amesema anaamini Man City watafanya vyema msimu huu na ikiwezekana wataweza kutwaa ubingwa wa Uingereza, baada ya kufanya usajili wa nguvu.

Katika hatua nyingine Craig Bellamy amesema ameamua kujiunga na klabu Cardiff City kwa lengo la kutaka kuwa karibu na familia yake.

No comments:

Post a Comment