KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, August 18, 2010

INAKERA SANA TABIA HII.


Meneja wa klabu ya Man Utd Sir Alex Ferguson amezionya klabu zinazotumia fedha kwa fujo kwa lengo la kufanya usajili wa wachezaji huku akizieleza katu ubingwa haunuliwi kwa fedha.

Sir Alex Ferguson ametoa onyo hilo, baada ya kuonekana kuchukizwa na hatua ya matumizi mabaya ya fedha yanayofanywa na wapinzani wake katika mji wa Manchester nchini Uingereza Man City ambao tayari wameshatumia zaidi ya paund million 150.

Mzee huyo toka nchini Scotland amesema klabu hizo zinatakiwa kufahamu suala la kutwaa ubingwa si la kutumia fedha nyingi kwa wakati mmoja bali ni suala la kujiandaa kwa muda mrefu hadi kufikia hatua ya kuwa na kikosi bora.

No comments:

Post a Comment