KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, August 25, 2010

KILA MMOJA ATACHEZA.


Meneja mpya wa klabu ya real Madrid Jose Mourinho amepanga kumpa nafasi kila mchezaji kwenye kikosi chake kinachohitaji kurejesha heshima huko Stantiago Bernabeu.

Mourinho amesema anaamini kila mchezaji katika kikosi chake ana uwezo wa kuchangia ushindi wa timu na akajihisi kuwa miongoni mwa walioleta mafanikio mwishoni mwa msimu endapo watafanikisha azma ya kutwaa vikombe.

Amesema lengo lake ni kurejesha heshima Stantiago Bernabeu ambayo imepoteza kwa kipindi cha miaka kadhaa hivyo kubwa kwa sasa ni kuweka mikakati ambayo itawafanya kufurahi kwa pamoja bila kumtenga yoyote yule.

Akimzungumzia Cristiano Ronaldo, meneja huyo wa kimataifa toka nchini ureno amesema mchezaji huyo bado ana ulazima wa kutumiwa katika eneo lingine uwanjani kwa lengo la kumpa uhuru wa uchezaji wake.

Mourinho ameongeza kuwa endapo mchezaji huyo atapatiwa mwanya wa kujitawala kwa nafasi yake atakuwa na ulazima wa kucheza na washambuliaji wengine waliopo klabuni hapo.

No comments:

Post a Comment