KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Sunday, August 22, 2010

KUYT APANIA KUTOKA LIVERPOOL.


Imeripotiwa kuwa mshambulaiji wa kimataifa toka nchini Uholanzi na klabu ya Liverpool Dirk Kuyt yu tayari kujiunga na klabu ya Inter Milan ya nchini Italia kwa lengo la kuwa sambamba na meneja wake wa zamani Rafael Benitez.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na wakala wa mshambuliaji huyo zimeeleza kuwa Dirk Kuyt ameonyesha dhamira hiyo kwa kumueleza wazi yu tayari kuondoka nchini Uingereza na kinachosubiriwa kwa sasa ni uwezekano wa viongozi wa klabu ya Inter Milan kukamilisha taratibu za kuanza mazungumzo ya kumsajili.

Hata hivyo wakala huyo amebainisha wazi kwa kusema kwamba siku ya Alkhamis usiku wakati wa mchezo wa Liverpool dhidi ya klabu ya Trabzonspor, toka nchini Uturuki uongozi wa klabu ya Inter Milan ulituma ofa ambayo ilimzuia meneja Roy Hodgson kutomtumia kwenye kikosi chake.

Tayari uongozi wa klabu ya Inter Milan umeshatangaza kutenga dau la paund million 15 ambalo linatarajia kutumika katika usajili wa mchezaji huyo aliejiunga na klabu ya Liverpool mwaka 2006 akitokea Feyenoord Rotterdam ya nchini kwoa Uholanzi.

No comments:

Post a Comment