KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, August 16, 2010

MARADONA ATAJWA VILLA PARK.


Gwiji wa soka nchini Argentina Diego Maradona amepigiwa upatu wa kujiunga na klabu ya Aston Villa iliyibaki mkiwa baada ya kuondokewa na meneja wake Martin O’Neil kati kati ya juma lililopita.

Nafasi hiyo kwa Maradona imezungumza na muwakilishi wa klabu ya Aston Villa barani ulaya Walter Soriano alipokuwa akihojiwa na muandishi wa habari wa gazeti la Sunday Mercury.

Walter Soriano amesema Diego Maradona huenda akawa wazi kujiunga na
klabu hiyo nakufikia melengo yaliyowekwa klabuni hapo hivyo wanasubiri utaratibu utakapotimia.

Mbali na Maradona kuzungumzwa pia meneja wa klabu ya Ajax Amsterdam Martin Jol pamoja na kocha mkuu wa timu ya taifa ya Marekani Bob Bradley nao wanatajwa kuchua nafasi ya Martin O’Neill ambayo kwa sasa inashikiliwa kwa muda na aliekua msaidizi wake Kevin McDonald ambae ameuanza vyema msimu kwa ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Aston Villa.

No comments:

Post a Comment