KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, August 25, 2010

Steven Jerome Pienaar KUBAKI GOODSON PARK.


Uongozi wa klabu ya Everton umekanusha taarifa za kuwa tayari kumuachia kiungo wa kimataifa toka nchini Afrika kusini winger Steven Jerome Pienaar kwa lengo la kujiunga na klabu ya Tottenham.

Taarifa hizo za uongozi wa klabu hiyo zimekanushwa na meneja msaidizi Steve Round ambae ameleeza kuwa kiungo huyo hawezi kuondoka kwa sasa kufuatia kuwa na mkataba ambao umesaliwa na muda wa mwaka mmoja.

Steve Round amesema dhumuni lao ni kutaka kumuona mchezaji huyo anasalia katika himaya ya Goodson Park yalipo makao makuu ya klabu ya Everton kwa ajili ya kuendelea kukiimarisha kikosi chao.

Steve Round pia maekanusha taarifa za klabu ya Everton kumsajili Peter Peter Crouch kama sehemu ya kubadilisha kwa wachezaji hao katika kipindi hiki.

Wakati huo huo meneja huyo msaidizi wa klabu ya Liverpool amezungumzia hatua ya kiungo wa kimataifa toka nchini Hispania Mikael arteta kuitwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza ambacho kinakabiliwa na michezo ya kufuzu kwa michuano ya mataifa ya ulaya mwaka 2012.

Steve Round amesema kuitwa kwa mchezaji huyo ama kutokuitwa ni jukumu la kocha mkuu Fabio Capello, na endapo Arteta atakubali wito huokwao itakua faraja kutokana na mchezaji huyo kutowahi kluitwa katika timu ya taifa ya Hispania.

No comments:

Post a Comment