KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, November 26, 2010

Aaron Ramsey AUZWA KWA MKOPO


Uongozi wa klabu ya Nottingham Forest umekamilisha taratibu za kumsajili kwa mkopo kiungo wa kimataifa toka nchini Wales na klabu ya Arsenal Aaron Ramsey alierejea uwanjani akitokea katika benchi la majeruhi huko jijini London.

Kukamilika kwa taratibu hizo za usajili wa mkopo, kutamfanya kiungo huyo kujiunga na Nottingham Forest Januari 3 mwaka 2011 huku kesho akitarajiwa kuwepo kwenye kikosi cha klabu yake ya Arsenal ambacho kitacheza na Aston Villa huko Villa Park.

Ramsey mwenye umri wa miaka 19, alifanikiwa kumaliza dakika 45 za mchezo wa wachezaji wa akiba kati ya Arsenal dhidi ya Walves, mchezo ambao ulikua unamrejesha uwanjani mara baada ya kupona jeraha lake ambalo alilipata mwezi wa pili mwaka huu.

Wakati Ramsey akitarajia kuelekea Nottingham Forest, uongozi wa klabu ya Dinamo Zagreb ya nchini Croatia umewatolea nje Arsenal ambao walituma ofa ya kutaka kuwasajili beki wa pembani Sime Vrsaljko pamoja na kiungo Mateo Kovacic.

Makamu wa raisi wa klabu ya Dinamo Zagreb Zdvravko Mamic amesema siku kumi zilizopita walikua na wajumbe wawili wa klabu ya Arsenal ambao waliwasilisha ofa hiyo lakini bila kuwaficha aliwakatalia kata kata.

Amesema wajumbe hao walifika klabuni hapo wakiwa na ofa ya kuwataka wachezaji hao kwa kiasi cha Euro million 20 (Paund million 16.9) lakini waliendelea kuwa na msimamo wao wa kukataa kuwauza wachezaji hao ambapo Vrsaljko ana umri wa miaka18, huku Kovacic akiwa na umri wa miaka 16.

No comments:

Post a Comment