KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, November 26, 2010

Wayne Rooney AENDELEA KUOMBA RADHI.


Mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Uingereza pamoja na klabu ya Man Utd Wayne Rooney amewataka radhi mashabiki, wafurukutwa na wakereketwa wa klabu hiyo kwa mchafuko uliojitokeza mwezi uliopita pale aliposhinikiza kuondoka huko Old Trafford.

Rooney ameomba radhi hizo ikiwa tayari amesharejea katika kikosi cha kwanza wa klabu ya Man Utd na kucheza michezo miwili ambayo yote kikosi cha klabu hiyo kimefanikiwa kupata ushindi.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 25, amewataka mashabiki wa soka wa klabu hiyo kusahau yaliyopita na kutazama yaliyo mbele yao ambapo kubwa ni kuhakikisha ubingwa wa soka nchini Uingereza unarejea mikononi mwao huku akitoa ahadi ya kuwa miongoni mwa wale watakao lifanikisha hilo.

Pia mshambuliaji huyo amewataka radhi wachezaji wenzake kwa kuwaleza kuwa yeye ni mwanaadamu kama walivyo wanaadamu wengine hivyo suala la kukosea ni la kawaida lakini hii leo anashukuru amerejea katika utaratibu mzuri wa kuitumikia klabu yake ipasavyo.

Wayne Rooney alizua sakata la kutaka kuondoka Man Utd baada ya kukataa kusaini mkataba mpya huku akihoji mustakabali wa klabu hiyo ambayo alidai imekosa muelekeo wa kiushindani.

Wengi walidhani Rooney huenda angejiunga na upande wa pili wa klabu za jiji la Manchester, (Man City) lakini alifikia hatua ya kubadili mawazo ya kuondoka klabuni hapo baada ya kufafanuliwa alichokua akikihitaji.

No comments:

Post a Comment