KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, November 26, 2010

JANJA YA MOURINHO YAJULIKANA !!!!



Shirikisho la soka barani Ulaya UEFA limebaini chanzo kilichopelekea wachezaji wa wawili wa klabu ya Real Madrid kuonyeshwa kadi nyekundu katika mazingira ya kutatanisha kwenye mchezo wa hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa barani Ulaya.

UEFA wamebaini chanzo hicho baada ya kufuatilia kwa ukaribu picha za televisheni za mchezo huo ambazo zimeonyesha mchezo mchafu uliofanywa na meneja wa klabu hiyo ya jijini Madrid Jose Mourinho kwa kushirikiana na wachezaji wake wane ambao ni Xabi Alonso, Sergio Ramos, Iker Casillas pamoja na Jerzy Dudek.

Kamati ya nidhamu iliyokua ikifuatilia mchezo huo mchafu kupitia picha za televisheni imebaini kuwa Mourinho alipeleka ujumbe kwa Xabi Alonso na Sergio Ramos ambao ndio wahanga wa adhabu za kadi nyekundu kupitia kwa kipa wake Jerzy Dudek ameonekana akizungumza na Iker Casillas.

Maamuzi rasmi ya kamati hiyo yanatarajiwa kutangazwa Novemba 30 ambapo yatatoa picha kamili kama wahusika hao wataadhibiwa ama la, na hii itakua baada ya wahusika kuitwa na kujitetea kwa tuhuma walizotupiwa.

Katika mchezo huo Xabi Alonso na Sergio Ramos walionekana wakisaka kadi nyekundu kwa makusudi kufuatia kitendo cha kuchelewa kupiga mpira kitendo ambacho kimetafsiriwa kama kupoteza muda wa mchezo huo ambao ulimalizika kwa Real Madrid kupata ushindi wa mabao manne kwa sifuri.

No comments:

Post a Comment