
Meneja wa klabu ya Man city Roberto Mancini amekanusha taarifa za mshambuliaji wa klabu hiyo Emmanuel Adebayor kuwa katika orodha ya kuuzwa kitakapofika kipindi cha usajili mwezi Januari mwaka 2011.
Mancini amekanusha taarifa hiyo zikiwa zimepita siku mbili baada ya msaidizi David Plat kubainisha wazi kwamba mshambuliaji huyo wa kimataifa toka nchini Togo yupo kwenye orodha ya kuuzwa klabuni hapo.
Mancini amesema hakuna ukweli wowote juu ya suala hilo na bado anaamini Emmanuel Adebayor ana uwezo mkubwa wa kuichezea klabu hiyo inayomilikiwa na tajiri wa kiarabu Sheikh Mansour bin Zayed Al Nahyan.
Hata hivyo menjeja huyo wa kiamataifa toka nchini Italia amemtaka Adebayor kuachana na fikra za kuondoka badala yake aelekeze akili yake huko City Of Manchester.
Katika taarifa iliyotolewa na David Plat ambayo ilihusiana na kuuzwa kwa Emmanuel Adebayor mwezi Januari pia iliwahusisha wachezaji wengine kama mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Paraguay Roque Santa Cruz pamoja na winga wa kiingereza Shaun Wright-Phillips.
No comments:
Post a Comment