KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, November 26, 2010

Ledley King KUMUONA MTAALAMU.


Nahodha na beki wa klabu ya Tottenham Ledley King mwanzoni mwa juma lijalo anatarajia kuelekea nchini Denmark kwa lengo la kuonana na mtaalamu wa kutibu maumivu ya nyonga yanayoendelea kumsumbua.

Beki huyo ambae kwa muda wa majuma kadhaa amekua nje ya kikosi cha klabu ya Spurs anatagemea safari hiyo huku akiwa na matumaini ya kurejea uwanjani siku za hivi karibuni kutokana na kuwa na imani mtaalamu anaekwenda kumuona ana uwezo mkubwa wa kumsadia kupona jeraha linalomsumbua.

Meneja wa klabu hiyo ya jijini London Harry Redknapp amezungumzana vyombo vya habari hii leo na kuthjibitisha uwepo wa safari hiyo ambayo amesema itatoa mustakabali mzuri kwa beki huyo kama ataweza kuwa Fit.

Amesema binafsi anaumizwa na kitendo cha kumkosa beki huyo kwenye kikosi chake ambapo mpaka sasa ameshamjumuisha kikosini mara saba tangu msimu huu ulipoanza kati kati ya mwezi August.

Katika hatua nyingine Harry Redknapp amesema kiungo wake wa kimataifa toka nchini Uingereza Jermaine Jenas hii leo alitarajiwaa kufanyiwa vipimo ambavyo majibu yake yatatoa taarifa kamili za muda gani kiungo atakuwa nje ya uwanja kufuatia maumivu ya kiazi cha mguu aliyoyapata kwenye mchezo w ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya Werder Bremen usiku wa kuamkia jana.

No comments:

Post a Comment