KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Saturday, November 27, 2010

MAN UTD WAPATA KIPA MPYA.


Hatimae klabu ya Man Utd imekamilisha taratibu za usajili wa klipa wa kimataifa toka nchini Denmark na klabu ya Aalesund Anders Lindegaard.

Man utd wamekamilisha dili la kumsajili kipa huyo huku malengo yao makubwa yakiwa ni kutaka kumrithisha nafasi ya kipa wa sasa Edwin van der Sar ambae tayari ameshatangaza kutundika gloves mwishoni mwa msimu huu.

Man Utd wamekamilisha dili hilo baada ya mazungumzo kati yao na uongozi wa klabu ya Aalesund ya nchini Denmark kukamilika siku mbili zilizopita ambapo mashetani wekundu walitakiwa kutoa kiasi cha paund million 3.5 kama ada ya uhamisho ambayo tayari imeshalipwa.

Hata hivyo kipa huyo mwenye umri wa miaka 26 atajiunga na klabu ya Man Utd kitakapofika kipindi cha dirisha dogo la usajili mwezi Januari mwaka 2011.

Meneja wa klabu Man Urd Sir Alex Ferguson amemwagia sifa kedekede kipa huyo huku akisema ana uwezo mkubwa ambapo anaamini utawasaidia katika harakati za kuziba nafasi ya Edwin van der Sar.

Wakati Ferguson akimsifia kipa huyo kipa wa zamani wa klabu ya Man utd Peter Schumacher ameuponda usajili huo huku akisema Anders Lindegaard hana uwezo wa kutosha wa kuitumikia klabu hiyo ipasavyo.

No comments:

Post a Comment