
Klabu ya Al Ahly ya nchini Misri imemtangaza mchezaji wa zamani wa klabu hiyo Abdel Aziz Abdel Shafi kuwa kocha wa muda wa klabu hiyo.
Uongozi wa klabu hiyo umemteua Abdel Aziz Abdel Shafi kuwa kocha wa muda kufuatia aliekua kocha klabuni hapo Hossam Al Badry, kutangaza kujiuzulu mwishoni mwa juma lililopita baada ya kukubalia kisago kutoka kwa Ismailia katika mchezo wa ligi.
Shafi ameteuliwa kushika nafasi hiyo ambapo atasaidiana na Sayed Abdel Hafeez, ambae anatarajiwa kuwa mkurugenzi wa mfundi wa chama cha soka nchini Misri.
No comments:
Post a Comment