
Chama cha soka nchini Scotland kimelaani vitendo vya kuwatishia maisha waamuzi wanaochezesha michezo ya ligi kuu nchini humo.
Kauli hiyo imetolewa na George Peat ambae ndie raisi wa chama hicho ambapo amesema amesikitishwa na hatua ya manyanyaso na vitisho vinavyotolewa dhidi ya waamuzi hao ambao jana walitangaza kugoma kuchezesha michezo ya mwishoni mwa juma hili.
George Peat pia ameeleza kusikitishwa na mgomo uliotangazwa na waamuzi hao hatua ambayo imemfanya yeye pamoja na jopo lake la uongozi kuanza kukibembeleza chama cha waamuzi nchini Scotland ili kiweze kulegeza msimamo huo.
Amesema wanajitahidi kwa hali mali kuhakikisha burudani ya soka mwishoni mwa juma hili inakuwepo huku pia akiwataka mashabiki kukoma kutoa vitisho na masimango kwa waamuzi wanapokua ndani na nje ya uwanja .
Uamuzi wa waamuzi wa soka nchini Scotland kugoma ulifikiwa kwenye mkutano wa chama cha waamuzi uliofanyika siku ya Jumapili mchana.
Sakata hilo la waamuzi kunyanyaswa na kutishiwa maisha limechukua mkondo wake kufuatia baadhi ya waamuzi kushindwa kutoa haki wanapokua uwanjani hatu ambayo inawachukiza mashabiki wa vilabu vinavyoonewa.
No comments:
Post a Comment