KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, November 24, 2010

Zeljko Petrovic AVUNJA NDOA NA WEST HAM UTD.


Meneja msaidizi wa klabu ya West Ham Zeljko Petrovic ametangaza kujiondoa kwenye klabu hiyo inayoshika mkia katika msimamo wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza.

Taarifa toka ndani ya klabu hiyo ya jijini London zimeeleza kuwa Zeljko Petrovic ameondoka klabuni hapo kwa utashi wake binafsi hivyo uongozi wa The Hummers umemtakia kila la kheri katika maisha yake mara baada ya kuondoka huko Upton Park.

Licha ya taarifa hizo kueleleza Zeljko Petrovic ameondoka kwa utashi binafsi, pia tetesi zinaeleza kwamba meneja huyo msaidizi kutoka nchini Yugoslavia amelazimika kuondoka kufuatia kuchukizwa na matokeo mabovu yanaendelea kupatikana ndani ya kikosi cha klabu hiyo ambacho mpaka hii kleo kimeshinda mchezo mmoja kati ya michezo 14 ya ligi waliyocheza chini ya meneja Avram Grant.

Kubwa linalosemekana kumkera mno Zeljko Petrovic mwenye umri wa miaka 45 ni hatua ya kupoteza mchezo wa mwishoni mwa juma lililopita mbele ya klabu ya Liverpool ambayo iliibuka na ushindi wa mabao matatu kwa sifuri.

Kuondoka kwa meneja huyo msaidizi tayari kumeshaanza kuzua tetesi zinazoeleza kwamba nafasi yake huenda ikazibwa na mshambuliaji wa zamani wa klabu hiyo ya Paolo Di Canio ambae ameshawasilisha maombi.

No comments:

Post a Comment