
Beki wa klabu ya Newcastle Utd Mike Williamson huenda akaadhibiwa na chama cha soka nchini Uingereza kufuatia tukio alilolifanya kwenye mchezo wa mwishoni mwa juma lililopita la kumpiga kichwa mshambuliaji wa klabu ya Bolton Wanderers Johan Elmander.
Msemaji wa FA amesema kamati ya nidhamu ya chama hicho linachunguzwa tukio lililofanywa na Mike Williamson kupitia picha za televisheni na kama itathibitika alimpiga Johan Elmander kwa makusudi adhabu yake itawekwa hadharani.
No comments:
Post a Comment