
Siku kadhaa baada ya kuthibitisha huenda akaondoka kwenye klabu ya Blackburn Rovers endapo atapata ruhusa ya meneja wa klabu hiyo Sam Allardyce, mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Grenada Jason Roberts hatoondoka tena ndani ya klabu hiyo.
Safari ya mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 32 ya kuondoka klabuni hapo mwezi januari mwaka 2011 kama alivyoeleza, imefifishwa na meneja wake Big Sam baada ya kukaata kumpa ruhusa aliyoiwasilisha siku tano zilizopita.
Jason Robert amesema kufuatia hali hiyo hana budi kuendelea kubaki huko Ewood Park licha ya kusikitishwa na kitendo cha kukatishiwa ndoto zake za kucheza nje ya Blackburn ambapo anadhani huenda angepata nafasi ya kucheza kila juma.
Hata hivyo ameeleza kwamba kunyimwa ruhusa ya kuondoka huenda ikawa ni faraja kubwa sana kwake ya kupata nafasi ndani ya kikosi cha klabu cha Blackburn Rovers ambacho mwishoni mwa juma hili kitakua nyumbani kikicheza na Aston Villa.
Jason Robert alikua akifikiria kuondoka klabuni hapo baada ya kukiri kuchoshwa na kitendo cha kukaa benchi kwa muda mrefu hatua ambayo anaamini endapo akisajiliwa na klabu nyingine kuna uwezekano mkubwa wa kuchezeshwa kila juma.
No comments:
Post a Comment