
Meneja wa klabu ya Stoke City Tony Pulis amesema chama cha soka nchini Uingereza kinalazimika kutoa mchango mkubwa wa matibabu ya wachezaji walioumia wanapokua kwenye michezo ya kimataifa ya kirafiki.
Tony Pulis ametoa rai hiyo kwa viongozi wa chama cha soka kufuatia kuumia kwa nahodha na kiungo wa klabu ya Liverpool Steven Gerrard alipokua kwenye mchezo wa jana wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya timu ya taifa ya Ufaransa iliyoibuka na ushindi wa mabao mawili kwa moja.
Amesema endapo chama cha soka kitaingilia kati suala hilo na kuwajibika kikamilifu uongozi wa vilabu hautokua ukilalamika juu ya gharama ambazo wanaingia kuwatibu wachezaji wanaporejea kutoka kwenye timu ya taifa wakiwa wameumia.
Hata hivyo kauli hiyo ya meneja wa klabu ya Stoke City imepingwa vikali na kocha mkuu wa timu ya taifa ya Uingereza Fabio Capello ambapo amesema ina muelekea mzuri kwa vilabu kua na uhakika na wachezaji wao, lakini itamnyima haki ya kuwa na wachezaji mahiri na walio komaa kama Gareth Barry, Rio Ferdinand pamoja na wengineo.
Katika mchezo wa jana nahodha na kiungo huyo wa klabu ya Liverpool alimaliza hukua kiwa na maumivu ya nyonga ambayo sasa yanamuweka kwenye benchi la majeruhi sambamba na mshambuliaji Ferdnando Torres anaeuguza jeraha la kifundo cha mguu.
Uongozi wa klabu ya Liverpool umetoa malalamiko yake juu ya kitendo hicho ambacho kimeonekana kuwakera mno huku ukieleza mzigo wa matibabu ya Gerarrd kwa sasa upo kwao nasi kwa viongozi wa chama cha soka nchini Uingereza walioandaa mchezo wa kirafiki.
No comments:
Post a Comment