
Shirikisho la soka duniani FIFA limetangaza kuwafungia wajumbe wawili wa kamati kuu ya shirikisho hilo Amos Adamu pamoja na Reynald Temarii baada ya kuwakuta na hatia ya kujihusishwa na masuala ya rushwa katika kipindi hiki cha kuyateua mataifa yatakayoandaa fainali za kombe la dunia za mwaka 2018 pamoja na 2022.
FIFA wametangaza adhabu kwa wajumbe hao baada ya kukamilika kwa uchunguzi uliofanywa na kamati ya nidhamu ya shirikisho hilo ambalo limekua likipiga vita kubwa ya rushwa katika mchezo wa soka ulimwenguni kote.
Akitangaza adhabu kwa wajumbe hao wawili mwenyekiti wa kamati ya nidhamu ya shirikisho hilo Claudio Sulser alipokutana na waandishi wa habari hii leo huko mjini Nyon nchini Uswiz yalipo makao makuu ya FIFA, amesema Amos Adamu amefungiwa kujishughulisha na masuala ya soka kwa kipindi cha miaka mitatu pamoja na kutozwa fainali ya Franga za Uswiz 10,000 ($10,200; £6,300).
Nae Reynald Temarii ambae ni raisi wa shirikisho la soka ukanda wa Oceania amefungiwa kwa kipindi cha mwaka mmoja pamoja na kutozwa faini ya Franga za Uswiz 5,000 ($ 5,100; £3,150).
Hata hivyo kamati hiyo imetoa nafasi kwa wafungwa hao kukata rufaa endapo hawatokubaliana na maamuzi yaliyotolewa dhidi yao.
Mara baada ya adhabu hizo kutolewa Amos Adamu kutoka nchini Nigeria amezungumza na vyombo vya habari na kueleza masikitiko yake ambapo amesema anashangazwa na hatua ya kufungiwa kwake ili hali hakujihusisha na suala hilo ambalo anadai limemchafua yeye, familia yake pamoja na nchi yake kwa ujumla.
Rungu hilo la adhabu pia limemuangukiwa mjumbe wa kamati kuu ya shirikisho la soka barani Afrika CAF Ismael Bhamjee kutoka nchini Botswana ambae alikua akituhumiwa kwa tuhuma za kulangua na kuuza tiketi za fainali za kombe la dunia za mwaka 2006 nchini kwao.
Ismael Bhamjee ameadhibiwa kwa kutokujhusishwa na masuala la soka kwa kipindi cha miaka miwili sambamba na kutozwa faini ya Franga za Uswiz 10,000.
No comments:
Post a Comment