KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Saturday, November 20, 2010

BLATTER ARIDHISHWA NA MAAMUZI.


Baada ya kamati ya nidhamu ya shirikisho la soka duniani FIFA kutoa adhabu kwa watuhumiwa ambao walikwenda kinyume na taratibu za shirikisho hilo, raisi Sepp Blatter, ametoa kauli ya kuridhishwa na maamuzi yaliyochukuliwa dhidi ya watuhumiwa hao.

Blatter ametoa kauli hiyo hukua kisema anatambua kuna baadhi ya mashabiki wa soka ulimwenguni huenda wakawa wamechukizwa na adhabu zilizoztangazwa juzi na kamati ya nidhamu lakini ukweli kwa upande wake amertidhika na adhabu hizo.

Amesema mbali na mashabiki wa sopka ulimwenguni kote pia wapo wajumeb wa kamati kuu ya FIFA ambao nao hawakufurahishwa na adhabi hizo zilizotolewa baada ya uchunguzi kufanywa kwa siku kadhaa na kubainika ni kweli watuhumiwa walioadhibiwa walikua na makosa kihalali.

Sepp Blatter amebariki adhabu hizo huku bara la afrika likiendelea kuikumbuka adhabu iliyotolewa kwa Amos Adamu kutoka nchini Nigeria, ya kufungiwa kujishughulisha na mchezo wa soka kwa miaka mitatu sambamba na kutozwa faini ya Franga za Uswiz 10,000 ambazo ni sawa na ($10,200; £6,300).

Amos Adamu aliadhibiwa adhabu hiyo baada ya kubainika aliomba rushwa ya fedha kwa moja ya nchi zinazotaka nafasi ya kunadaa fainali za kombe la dunia za mwaka 20018 hukua kitaka fedha hizo ambazo zingetumika kutegenezea viwanja vya nyasi bandia zipiwekwe kwenye akauti zenye majina ya watoto wake.

Mwingine aliaadhibiwa ni raisi wa wa shirikisho la soka ukanda soka ukanda wa Oceania Reynald Temarii ambae amefungiwa kwa kipindi cha mwaka mmoja pamoja na kutozwa faini ya Franga za Uswiz 5,000 ($ 5,100; £3,150).

Maafisa wengine wanne ambao zamani walikuwa katika kamati kuu ya FIFA walioangushiwa rungu hilo la adhabu ni pamoja na, Slim Aloulou wa Tunisia, Amadu Diakite kutoka Mali, Ahongalu Fusimalohi wa Tonga na Ismael Bhamjee kutoka Botswana.

No comments:

Post a Comment