
Meneja wa klabu ya Blackpool Ian Holloway ameendelea kuushambulia uongozi wa FA kufuatia sakata la kubadili kikosi chake kwa kuwajumuisha wachezaji 10 ambao hakuwahi kuwaanzisha katika michezo yua ligi msimu huu.
Holloway ameendelea kuuponda mfumo uliowekwa na uongozi wa chama hicho cha soka huku uchunguzi wa sakata hilo ukiendelea kufanywa na endapo itabainika alipanga kikosi dhaifu kwa kusudio la kuibeka klabu ya Aston Villa aliyocheza nayo kati kati ya juma
lililopita ataadhibiwa kwa kutozwa faini.
Amesema endapo FA watamtoza faini hiyo kwake itakua kama uonevu ambao pia utauathiri uongozi wa klabu hiyo ili hali kazi anayoifanya anaamini inaaminiwa na uongozi huo.
No comments:
Post a Comment