
Aliekua meneja msaidizi wa klabu ya Chelsea Ray Wilkins anajiapanga kuifikisha mahakamani klabu hiyo baada ya kupata ushauri toka ndani ya chama cha maneja wa vilabu nchini Uingereza ambacho kimebaini makosa aliyofanyiwa meneja huyo.
Ray Wilkins ambae aliarifiwa kuondoka klabuni hapo mnamo Novemba 11 mwaka huu mara baada ya mkataba wake kumalizika amesema uongozi wa klabu ya Chelsea ulifanya hatua hizo kwa uharaka zaidi ili hali walikua wanajua tayari kuna mazungumzo dhidi yake yalikua yakiendelea.
Amesema baada ya kuarifiwa kuondoka klabuni hapo alikwenda moja kwa moja kwenye chama cha mameneja wa vilabu nchini Uingereza na kusaka ushauri wa nini anachotakiwa kufanya na ndipo baadhi ya makosa yalibainika na alitakiwa kuundikia barua uongozi wa the Blues na kuuliza baadhi ya maswali, hatua mbayo amedai ameshaifanikisha.
Wilkins am,bae aliwahi kuichezea klabu ya Chelsea, Manchester United pamoja na Chelsea katika sehemu ya kiungo pia ameeleza kusikitishwa kwake na utaratibu wa kuelezwa taarifa za kutosaini mkataba mwingine klabuni hapo, huku akikiri aliishi vyema na kila mmoja huko Stamnford Bridge hatua ambayo aliona huenda ingempa nafasi kubwa ya kuendelea kubaki.
Hata hivyo ameutakia uongozi, wachezaji pamoja na mashabiki wa klabu ya Chelsea kila la kheri katika utaratibu wa kusaka namna ya kubakisha ubingwa wao wa Uingereza msimu huu ambao tayari umeshaanza kuonyesha kuwa na upinzani mkubwa kutoka kwenye vilabu tofauti.
Katika hatua nyingine mtendaji mkuu wa chama cha mameneja wa violabu nchini Uingereza Richard Bevan amethibitishwa taarifa za kulitafutia suluihu suala na Ray Wilkins lililobisha hodi ofisini kwao huku akisema tayari wameshampatia mwanasheria mbae atasaiodiana nae katika harakati za kusaka hali yake.
Wakati huo huo aliekuwa meneja wa klabu ya Chelsea Luiz Philippe Scolari amesema ameshangazwa na hatua zilizochukuliwa na uongozi wa klabui hiyo za kutoendelea na Ray Wilkins ambae alifanya nae kazi kwa ukaribu mno.
Luiz Philippe Scolari ambae kwa sasa nakionia kikosi cha klabu ya Palmeiras ya nchini kwao Brazil amesema bado kulikua na umuhimu mkubwa kwa klabu ya Chelsea kuendelea kuwa na Wilkins ambae amedai ana uwezo mkubwa wa ufundishaji huku akikiria meneja huyo wa kiingereza alimsaidia sana wakati akikiongoza kikosi cha Abramovic mwaka 2008-09.
No comments:
Post a Comment