KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, November 19, 2010

CHELSEA YAMPANDISHA CHEO SKAUTI WAKE.


Uongozi wa klabu ya Chelsea umempandicha cheo skauti wa klabu hiyo toka nchini Nigeria Michael Emenalo ambapo sasa atakua meneja msaidizi wa kikosi cha kwanza klabuni hapo.

Emenalo ambae alijiunga na klabu hiyo bingwa nchini Uingereza mwezi Oktoba, 2007 ametangazwa kushika madaraka hayo baada ya aliekua meneja msaidizi klabu ya Chelsea Ray Wilkins kumaliza mkataba wake mwanzoni mwa juma lililopita.

Michael Emenalo ambae bado anakumbukwa nchini kwao Nigeria kwa shughuli nzuri aliyoifanya alipokua akiichezea timu ya taifa ya nchi hiyo, licha ya kutajwa kuwa msaidizi wa Carlo Ancelotti amepewa uhuru wa kuendelea na shughuli yake ya uskauti endapo atapata nafasi mbali na madaraka aliyopewa.

No comments:

Post a Comment