KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, November 19, 2010

SAKATA LA GHANA LAMALIZIKA


Sakata la ahadi ya fedha walizoahidiwa wachezaji wa timu ya taifa ya Ghana baada ya kufika kwenye hatua ya robo fainali ya michuano ya kombe la dunia mwaka huu iliyofanyika nchini Afrika kusini limefikia kikomo.

Sakata hilo limefikia kikomo baada ya mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliochezwa usiku wa kuamkia jana kati ya timu ya taifa ya Ghana dhidi ya timu ya taifa ya Saudi Arabia ambao ulimalizika kwa sare ya bila kufungana.

Baada ya mchezo huo uongozi wa benki kuu ya nchini Ghana ulikabidhi hundi ya dola za kimarekani 63,000 ambazo zitagaiwa kwa wachezaji wote 23 waliokwenda nchini Afrika kusini na kufanya vyema katika fainali za kombe la dunia.

Sakata la fedha hizo ambazo ziliahidiwa na uongozi wa benki hiyo limekua likizungumzwa sana katika vyombo vya habari nchini Ghana ambapo wachezaji wote 23 walikua wakitaka kulipwa kwa mfumo wa pesa taslimu na si hundi hali ambayo ilizua tafrani kwa kuhisi huenda wachezaji hao wasingezipata fedha hizo.

No comments:

Post a Comment