KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, November 23, 2010

ETO'O AMMATERAZI MCHEZAJI WA CHIEVO VERONA.



Chama cha soka nchini Italia kimetangaza kumfungia michezo mitatu mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Cameroon pamoja na klabu ya Inter Milan Samuel Eto'o baada ya kamati ya nidhamu ya chama hicho kumkuta na hatia.

Samuel Eto’o amekutwa na hatia hiyo baada ya uchunguzi wa picha za televisheni kufuatiliwa kwa ukaribu zaidi na kubainika alimpiga kichwa kwa makusudi beki wa klabu ya Chievo Verona Bostjan Cesar pale timu hizo zilipokutana mwishoni mwa juma lililopita.

Katika mchezo huo ambao ulishuhudia Inter Milan wakibamizwa mabao mawili kwa moja, Samuel Eto’o alifikia hatua ya kumpiga kichwa cha kifuani Bostjan Cesar baada ya kuchukizwa na kitendo cha kupigwa shingoni na beki huyo ambae alikua na jukumu la kumkaba.

Hata hivyo kitendo hicho kilichofanywa na Eto’o hakikuonekana na muamuazi wa mchezo huo na endapo kingeonekana, mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 29 angeadhibiwa kwa kuonyeshwa kadi nyekundu.

Kufungiwa kwa Samuel Eto’o kumeendelea kumuweka juu ya mawe meneja wa klabu ya Inter Milan Rafael Benitez ambae safu yake ya ushambuliaji inaendelea kuwa butu kufuatia mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Argentina Diego Milito kuwa majeruhi.

No comments:

Post a Comment